Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ashiriki NBC Marathon Dodoma
Sisti Herman
July 28, 2024
Share :
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa leo Julai 28, 2024 ameshiriki katika mbio za hisani za Benki ya NBC zilizoanzia na kuishia katika uwanja wa mpira wa miguu wa Jamhuri jijini Dodoma.
Mheshimiwa Majaliwa ameipongeza benki hiyo kwa kaundaa mbio hizo zenye lengo la kusaidia mapambano dhidi ya saratani ya shingo ya kizazi kwa wanawake.
Pia mbio hizo zimelenga kuchangia ujenzi wa chumba cha upasuaji katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.