Waziri Mkuu Slovakia afanyiwa upasuaji baada ya kupigwa risasi
Eric Buyanza
May 16, 2024
Share :
Waziri Mkuu wa Slovakia Robert Fico hayuko tena katika hali ya kuhatarisha uhai wake baada ya kujeruhiwa vibaya kwa risasi za tumbo hapo jana.
Naibu Waziri mkuu wa nchi hiyo, Tomas Taraba aliiambia BBC kuwa upasuaji aliofanyiwa Bw Fico umeenda vizuri na kuna uwezekano mkubwa wa yeye kupona.
Mshukiwa wa tukio hilo alikamatwa kwenye eneo la tukio.