Waziri Mkuu wa Kongo ajiuzulu
Eric Buyanza
February 21, 2024
Share :
Waziri mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Jean-Michel Sama Lukonde amejiuzulu, hatua inayosababisha kuvunjwa serikali yake. Amejiuzulu siku nane baada ya kuidhinishwa kwa nafasi yake kama mbunge wa kitaifa.
Sasa atahudumu bungeni katika nafasi ya ubunge. Ofisi ya rais imesema ombi lake la kujiuzulu limekubaliwa. Hata hivyo, rais ameiomba serikali ya Lukonde kuendelea kuyashughulikia masuala ya sasa hadi pale serikali mpya itakapoundwa.
Lukonde aliteuliwa kuwa waziri mkuu mwaka 2021 akiwa na miaka 43, akimrithi aliyekuwa Waziri Mkuu Sylvestre Ilunga Ilunkamba, ambaye alijiuzulu baada ya wabunge kupitisha kura ya kutokuwa na imani naye.