Waziri mkuu wa mali auawa kwa bomu la kutegwa
Eric Buyanza
April 27, 2026
Share :

Utawala wa kijeshi nchini Mli umetangaza siku mbili za maombolezo ya kitaifa Jumapili, Aprili 26, baada ya kuthibitisha kifo cha Waziri wa Ulinzi Sadio Camara, aliyeuawa nyumbani kwake huko Kati wakati wa mashambulizi ya Aprili 25.
Kaskazini mwa nchi, waasi wa Tuareg, wanaoungwa mkono na makundi ya wanajihadi, wamechukua udhibiti kamili wa jiji la Kidal, ambapo mamlaka ya kiraia na kijeshi ya Mali zimeamua kuondoka, kama vile wanamgambo wa kundi la mamluki la Urusi la Africa Corps, kufuatia mazungumzo.
Msemaji wa serikali ya Mali ametangaza siku mbili za maombolezo ya kitaifa, akizungumza Jumapili, Aprili 26, kwenye kipindi cha habari cha jioni cha televisheni ya seerikali ya ORTM. Msemaji huyo, Brigedia Jenerali Issa Ousmane Coulibaly, ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Ndani, amethibitisha kifo cha Waziri wa Ulinzi Sadio Camara katika shambulio la gari lililotegwa bomu. Ameelezea kwamba mlipuko huo pia ulisababisha kuanguka kwa majengo yaliyo kuwa karibu, ikiwa ni pamoja na msikiti, na kuua waumini kadhaa. Utawala wa kijeshi pia umetangaza siku mbili za maombolezo ya kitaifa.
Wakati hu huo utawala wa kijeshi umedai kuwaua "magaidi" 200 naumedai kwamba mashambulizi hayo yalilenga maeneo saba kwa jumla: Bamako na Kati, karibu na mji mkuu; Konna, Mopti, na Sévaré, katikati mwa nchi; na Gao na Kidal, kaskazini. Mkuu wa Jeshi ameelezea hali hiyo kama "ya wasiwasi sana mnamo Aprili 25" na akaielezea kama "mpango mkubwa na mgumu wa uvunjifu wa utulivu," huku pia akisema kwamba washambuliaji walirejeshwa nyuma.
Hata hivyo mji wa kaskazini wa Kidal uko chini ya udhibiti kamili wa wanajihadi wa JNIM na kundi la waasi la Tuareg FLA. Kufuatia mazungumzo, mamluki wa Urusi wa Africa Corps na jeshi la Mali waliondoka katika mji huo wakielekea Gao, kama vile mamlaka rasmi ya raia. Utawal wa kijeshi unazungumzia kujipanga upya nje ya Kidal, na hivyo kukiri kutokuwepo katika mji huo.





