pmbet

Waziri Mkuu wa Uingereza aipongeza Arsenal

Eric Buyanza

May 20, 2026
Share :

Waziri Mkuu wa Uingereza Sir Keir Starmer ameweka pembeni matatizo yake ya kisiasa ili kusherehekea ushindi wa timu yake ya Arsenal kutwaa ligi kuu ya soka nchini humo.

 

Arsenal walitawazwa mabingwa wa Uingereza kwa mara ya kwanza baada ya miaka 22, Jumanne usiku wakati Manchester City ikitoka sare na Bournemouth, hivyo alama zake hazitoweza kufikiwa na matajiri hao wa jiji la Manchester.

 

Starmer, ambaye anakabiliwa na shinikizo kubwa la kujiuzulu wadhifa wake, aliacha kuhudhuria sherehe za aina yoyote, lakini alipongeza kwenye mitandao ya kijamii.

 

Aliandika kwenye X: 'Miaka 22 mirefu kwa Arsenal. Lakini hatimaye, tumerudi pale tunapostahili. Mabingwa!'

Starmer anatarajiwa kuachia ngazi muda wowote, lakini inaelezwa anataka kufanya hivyo kwa masharti yake binafsi badala ya kulazimishwa na chama chake.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet