Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer atangaza kujiuzulu
Eric Buyanza
June 22, 2026
Share :
Baada ya shinikizo la wiki kadhaa kutoka kwa wapinzani wake, hatimae Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer ametangaza kujiuzulu.
Starmer amesema kiongozi mpya atatakiwa awe ameshaingia kazini kabla ya kurejea kwa Bunge mwezi Septemba.
Kabla ya kutangaza kujiuzulu, Starmer alisema alirithi Chama cha Labour "kilichofilisika kisiasa, kifedha na kimaadili".
Anasema alibadilisha chama kwa "kung'oa sumu ya chuki dhidi ya Wayahudi".
"Kurejesha imani kwa uchumi, ulinzi na usalama wa taifa".
Starmer anasema baada ya kuacha kazi hiyo atatumia muda wake mwingi kuwa mume bora kwa mke wake, na kuwa baba bora kadri awezavyo kwa watoto wake.






