Waziri silaa arejesha nyumba ya mjane aliyoporwa na mpangaji
Eric Buyanza
April 25, 2024
Share :
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe . Jerry Silaa amemrejeshea nyumba yake Bi. Zubeda Alawi Athumani ambaye ni Askari msataafu baada ya kuporwa nyumba ya marehemu mume wake na mfanyabiashara maarufu Jijini Tanga Anthony Adam Mmasi.
Waziri Silaa amefanya maamuzi hayo jana jioni alipotembelea nyumba hiyo ilipo eneo la Sahare karibu na Hoteli ya Tanga Beach baada ya kupokea malalamiko ya mama huyo akiwa na mwanae wakati wa Kliniki ya Ardhi inayoendelea jijini humo.
Aidha, Bi Zubeda Alawi Athumani na mwanae wamemshukuru Waziri Silaa kwa utendaji wake wa zingatia haki na usawa katika utatuzi wa migogoro ya ardhi.