pmbet

Waziri wa mambo ya nje wa Iran uso kwa uso na Putin

Eric Buyanza

April 27, 2026
Share :

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Abbas Araghchi amewasili nchini Urusi, ambapo atakutana na Vladimir Putin katika juhudi za kutafuta suluhu ya mzozo wake na marekani pamoja na Israel.

 

Hatua hiyo inakuja baada ya majadiliano kadhaa ya kidiplomasia kukwama.

Juhudi za kuanzisha tena mazungumzo kati ya Tehran na Washington zilipata pigo siku ya Jumamosi baada ya Rais wa Marekani Donald Trump kufuta safari ya wajumbe wake, Steve Witkoff na Jared Kushner, waliotarajiwa kwenda Islamabad kwa mazungumzo hayo.
 

Trump alieleza kupitia Fox News kwamba ikiwa kweli Iran inataka mazungumzo, "wanaweza kuja kwetu, au wanaweza kutupigia simu," akisisitiza kuwa Marekani haitashiriki mazungumzo yasiyo na tija.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet