pmbet

Wema Sepetu akanusha taarifa za kufariki dunia.

Joyce Shedrack

July 14, 2025
Share :

Staa wa maigizo na mshindi wa taji la Miss Tanzania mwaka 2006, Wema Sepetu, amelaani vikali taarifa za uzushi zilizosambazwa mitandaoni zikidai kuwa amefariki dunia.

 Kupitia ukurasa wake rasmi wa Instagram, Wema ameonyesha kuchukizwa na taarifa hizo ambazo amezitaja kuwa ni za kupotosha.

Wema aliposti picha iliyoonesha kichwa cha habari cha kughushi kilichoandikwa “Wema Sepetu afariki”, na kuandika ujumbe mzito kupinga uvumi huo.

“Kumbe nimefariki na sijui... Whoever that made this, Mungu anakuona... Fake News...!!! Mtakuja kuumiza watu wanaonipenda kwa Pressure...” ameandika Wema Sepetu.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet