Wenger hajaniandika kwasababu hajanifunga - Mourinho
Sisti Herman
January 7, 2024
Share :
Kocha mtata zaidi Jose Mourinho aliyewahi kuwa kocha wa Chelsea, Madrid na Man Utd alipoulizwa kwenye moja kati ya mahojiano kuhusu kwanini kwanini hajaandikwa kwenye kitabu cha maisha ya Arsene Wenger, Majibu yake yalikua hivi
"Kwasababu hajawahi kunifunga. Huwezi kuandika kurasa za kuelezea mechi 12 au 14 ambazo zote umefungwa, sasa kwanini aniandike kwenye kitabu chake?"
"Kitabu ni kitu cha kukisoma na kukifurahia na kujifanya ujivunie kwahiyo ninaelewa hali anayopitia."