Wepesi na kasi ya kinda wa Man United Kobbie Mainoo yawavutia wengi
Eric Buyanza
March 25, 2024
Share :
Kiungo wa kati Kobbie Mainoo ameitwa kwa mara ya kwanza kwenye kikosi cha England baada ya kufanya vizuri msimu huu akiwa na Manchester United.
Kinda huyo mwenye umri wa miaka 18, awali aliachwa katika kikosi cha Gareth Southgate katika mechi za kirafiki dhidi ya Brazil na Ubelgiji.
Majeraha na ukosefu wa wachezaji vilifungua milango kwa Mainoo kupata nafasi katika mipango ya Erik ten Hag mwishoni mwa 2023 - alipojitokeza kwa mara ya kwanza katika mechi dhidi ya Everton mwezi Novemba.
Mchambuzi wa soka wa BBC na mchezaji wa zamani wa Arsenal, Ian Wright anasema kijana huyo ameonyesha ukomavu wa hali ya juu katika mazingira magumu ambayo hayajonekana kwa mchezaji wa Uingereza kwa muda mrefu. Ninavutiwa kila ninapomtazama." alisema Wright.
Wepesi na kasi ya Mainoo viliwavutia wachambuzi wengi siku ya Jumapili alipokuwa akiwapita wachezaji watatu wa Liverpool ili kutengeneza nafasi dakika ya 34 kwa Scott McTominay katika mechi waliyoshinda 4-3.