Wes Brown haamini kama Ronaldo atarudi Man Utd
Sisti Herman
February 5, 2026
Share :

Wes Brown, amebainisha wazi kuwa Cristiano Ronaldo hawezi kurejea Machester United kwa mara ya tatu.
Beki huyo wa zamani wa kati wa Uingereza na Manchester United amesema kuna machaguo mengi kwa mshindi huyo mara 5 wa Ballon d’Or ya kufanya.
Brown amesema "kuhusu kurejea Manchester United?Ningesema hapana
"Sioni jinsi hilo lingeweza kutokea. Kuhamia MLS? Labda. Labda angerudi Ureno na kucheza huko. Nina uhakika bado atakuwa na chaguzi nyingi.Jambo kuu ni kwamba bado anataka kucheza Kombe la Dunia na tungelazimika kuendelea kucheza na kuhakikisha anajiweka sawa ili kufanya hivyo.
"Ni mshtuko kwa kila mtu kumuona Ronaldo akigoma lakini kwa kweli nadhani itatatuliwa. Tutalazimika kusubiri na kuona itaenda wapi kuanzia hapa."
Ronaldo mweye umri wa miaka 40 amekuwa na mgomo na klabu yake mapema wiki hii ikiripotiwa kutoridhika na usimamizi wa Mfuko wa Uwekezaji wa Umma wa Saudi Arabia (PIF), ikisemekana inapendelea klabu pinzani kifedha zaidi katika udhamini wao.





