pmbet

WFP na Sudan Kusini wazindua mfumo wa kukabiliana na ukame.

Joyce Shedrack

July 11, 2026
Share :

Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) kwa kushirikiana na Serikali ya Sudan Kusini limezindua mpango wa kwanza nchini humo wa kuchukua hatua za mapema dhidi ya ukame unaotarajiwa, huku hatari ya ukame ikizidi kuongezeka katika jimbo la Eastern Equatoria.

UN's WFP investigating collusion of staff with Sudan army in blocking aid |  | AW

Mpango huo, uliotangazwa Ijumaa kwa ufadhili wa Umoja wa Mataifa, unalenga kuwasaidia zaidi ya watu 65,000 wanaoishi katika kaunti za Budi na Kapoeta Kaskazini kabla ya athari kubwa za ukame kujitokeza.

 

Kwa mujibu wa WFP, hatua za mapema (Anticipatory Action) ni mfumo unaowezesha misaada ya kibinadamu kutolewa kabla ya janga kutokea, badala ya kusubiri madhara yaanze kujitokeza. Lengo ni kulinda maisha ya watu, kuimarisha usalama wa chakula na kuhifadhi vyanzo vyao vya kipato.

 

Mpango huo unatarajiwa kusaidia jamii zilizo katika hatari kukabiliana vyema na athari za ukame, kupunguza uharibifu wa maisha na mali, pamoja na kuongeza uwezo wa wananchi kustahimili majanga yanayosababishwa na mabadiliko ya tabianchi.

 

Uzinduzi wa mpango huu unaashiria hatua muhimu kwa Sudan Kusini katika kuimarisha mifumo ya tahadhari na maandalizi ya kukabiliana na majanga ya ukame kabla hayajaleta athari kubwa kwa jamii zilizo hatarini.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet