Whozu kwenye Bongo Movie hapana - Wema sepetu
Eric Buyanza
May 27, 2024
Share :
Wakati wengi wakitamani au kufikiri ya kwamba iko siku mwigizaji Wema Sepetu atamkaribisha mpenzi wake Whozu kunako tasnia ya Bongo Movie, mrembo huyo ambaye wengi humtambua kwa jina la 'Tanzania Sweetheart' ameibuka na kusema hadhani kama hilo litatokea.
Wema anasema anapenda sana kumuona mpenzi wake Whozu akiwa kwenye muziki na hajawahi kufikiria kumtoa huko na kumuingiza Bongo Movie, na kusisitiza kama Whozu ataacha muziki basi ni bora akajiingiza kwenye shughuli zingine lakini sio Bongo Movie.