Wiki ijayo lazima tushinde, hata ikibidi tufe uwanjani - Kompany
Eric Buyanza
April 29, 2026
Share :
Kocha wa Bayern Munich, Vincent Kompany ametoa wito kwa mashabiki wa klabu hiyo ikiwa ni masaa machache baada ya kupoteza mchezo kwa bao 5-4 dhidi ya PSG:
"Ombi langu pekee ni kwamba ikiwa kuna mtu alinunua tiketi na kujisikia vibaya siku ya mchezo, kaa nyumbani na uigawe tiketi yako kwa watu walio fiti na uwezo wa kushangilia ndani ya ngome yetu ambayo ni Allianz Arena. Lazima tushinde mchezo na tunahitaji sapoti ya watu 75,000 uwanjani.
Hali ya hewa wiki ijayo ndani ya Allianz Arena itakuwa ya kichaa. Tunajua tunapaswa kushinda. Tutajitoa kwa kila kitu...hata ikibidi tufe uwanjani." alimalizia kocha huyo wa kibelegiji.






