William Ruto Mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki 'EAC'
Joyce Shedrack
November 30, 2024
Share :
Rais wa Kenya William Ruto ametangazwa rasmi kuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki(EAC) akichukua nafasi hiyo kutoka kwa Rais wa Sudan Salva Kiir Mayardit ambaye amemaliza muda wake.
Ruto ametangazwa leo hii katika Mkutano wa 24 wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) uliofanyika Jijini Arusha kwenye ukumbi wa mikutano AICC.