Winga alivyowaua Ureno na kuomba jezi ya Ronaldo
Eric Buyanza
June 27, 2024
Share :
Baada ya kuwafunga Ureno kwenye mchezo wa raundi ya tatu ya hatua ya makundi ya kombe la mataifa Ulaya (Euro) kundi F, Georgia wakishinda 2-0, winga wa timu hiyo Khivcha Kvaratskhelia hakutaka kupitwa na ndoto ya kubadilishana jezi na mchezaji wake bora wa dunia wa muda wote, Cristiano Ronaldo.
Baada ya mchezo winga huyo hatari wa Napoli ya Italia alichapisha picha kupitia mitandao yake ya kijamii ikionyesha jezi aliyochezea Ronaldo na ujumbe uliosomeka "Dreams" akiambatanisha na tuzo ya mchezaji bora wa mchezo huo.
Ureno na Georgia wamefuzu hatua ya mtoano kwenye kundi hilo baada ya kukusanya alama nyingi zaidi.