pmbet

Winga aliyehitajika Simba asaini Ihefu

Sisti Herman

April 15, 2024
Share :

Mwandishi wa kujitegemea wa habari za michezo hasa masuala ya usajili kutoka nchini Ghana, Micky Jr amethibitisha kuwa klabu ya Ihefu (Singida Black Stars) imekamilisha usajili wa aliyekuwa winga wa US Gendamarie ya Niger na RS Berkane Victorien Adebayor ambaye aliwaniwa na Simba misimu miwili iliyopita.

Adebayor ambaye kipindi cha nyuma aliziingiza vitani Simba na Vigogo wa Morocco RS Berkane baada ya kunaswa na wa Morocco hao hakuwa na kiwango bora kabla ya kukaa nje ya uwanja kwa muda mrefu kwa majeraha kisha kusaini mkataba na Amazulu ambako nako hakutumikia mkataba huo mpaka sasa.

Ihefu imekuwa na kisu kikali kwenye soko la usajili ikipigana vikumbo na vilabu vikubwa vya nchini kama Simba na Yanga na vile vya kimataifa.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet