Winga Simba atinga jezi ya 'Taifa Stars' mazoezini Ivory Coast
Sisti Herman
June 6, 2024
Share :
Winga wa klabu ya Simba Aubin Kramo raia wa Ivory Coast akiwa mapumzikoni kwao kwaajili ya maandalizi ya msimu ujao, ameonekana akiwa kwenye mazoezi ya klabu yake ya zamani Asec Mimosas huku akiwa ametinga jezi ya timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars'.
Kramo ambaye hajapata nafasi ya kucheza Simba kwasababu ya kusumbuliwa na majeraha msimu mzima ameripotiwa kuwa fiti kwaajili ya msimu ujao baada ya kuuguza na kupona majeraa yake.