Winga Stras gumzo Misri
Sisti Herman
January 8, 2024
Share :
Licha ya Timu ya Taifa Tanzania 'Taifa Stars' kukubali kichapo cha mabao 2-0 kutoka kwa Misri kwenye mechi ya kirafiki kujiandaa na AFCON iliyopigwa jana Cairo mashabiki wengi wamekoshwa na Tarryn Allarakhia ambaye alikiwasha sana kwenye ubavu wa kushoto baada ya kuingia kipindi cha pili.
Mechi hiyo imetumika kupimana kwa vikosi vyote viwili ambavyo vinashiriki fainali za Afcon 2023 zitakazoanza Januari 13 nchini Ivory Coast.
Mabao ya Misri yamefungwa na Mahmoud Trezeguet dakika ya 32 na Aisha Manula akijifunga dakika ya 73.