pmbet

Winga wa sauzi akataliwa Morocco kwa uvutaji wa bangi

Sisti Herman

July 7, 2025
Share :

 

Aliyekuwa winga wa Kaizer Chiefs ya Afrika kusini Kgaogelo Sekgota ameshindwa uhamisho wake wa kutua katika klabu mojawapo nchini Morocco kutokana na tatizo la matumizi ya bangi.

Winga huyo wa zamani wa Kaizer Chiefs alivutiwa na klabu moja ya Morocco kabla ya kupelekwa katika kituo cha kurekebisha tabia nchini Afrika Kusini.

Haya yamefichuliwa na Watson Luandi, Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Urekebishaji cha Hope of Achievers huko Limpopo.

Luandi alithibitisha kuwa Sekgota ni mmoja wa wachezaji watatu wanaoendelea na matibabu katika kituo hicho, pamoja na kiungo wa zamani wa Bafana Bafana, Lerato Chabangu na Yamkela Phalane.


 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet