pmbet

Wisdom International Tournament 2024 ya Fountain Gate kuwakusanya Dodoma maskauti wa timu za Ulaya

Sisti Herman

May 30, 2024
Share :

Msimu mpya wa Wisdom Tournament 2024 inatarajia kuanza kutimua vumbi Juni 15  mwaka huu Dodoma unatarajiwa kuwa moto zaidi ya misimu iliyopita.

 

Hiyo ni Kwa mujibu wa C.E.O wa Fountain Gate Sports Academy Kelvin Shaban Kheri wakati akizungumzia mipango ya maandalizi yalipofika, akisema timu 70 kutoka Mataifa mbalimbali zikitarajia kushiriki.

 

"Huu ni mwaka wa utofauti kwenye Mashindano ya Wisdom ambayo yanawalenga wachezaji vijana zaidi kutoka maeneo mbalimbali.

 

"Timu 70, wachezaji zaidi ya 1,000 na maskauti kutoka sehemu mbalimbali watakuwa sehemu ya Mashindano haya makubwa nchini Kwa vijana. Hii ni fursa na Kwa wachezaji Wote ya kuweza kusogea na kwenda mbali zaidi," alisema Kelvin.

 

Mashindano hayo yanatarajiwa kufanyika Kwa siku tano na Moja kati ya Wadau watakaokuwepo kutazama Mashindano hayo ni pamoja na Shafiih Dauda Frank Petersen raia wa Denmark.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet