Wiz Khalifa akamatwa nchini romania baada ya kuvuta bangi jukwaani
Eric Buyanza
July 15, 2024
Share :
Rapa maarufu wa Marekani Wiz Khalifa alikamatwa jana Julai 14 nchini Romania baada ya kukutwa na madawa ya kulevya aina ya Bangi.
Rapa huyo ambaye jina lake halisi ni Cameron Thomaz, alikuwa Romania kwa ajili ya kushiriki tamasha la "Beach, Please!" lililofanyika kwenye pwani ya Costinesti na inaelezwa kuwa alionekana akivuta bangi wakati akiwa jukwaani.
Baada ya kukamatwa Khalifa alikutwa na zaidi ya gramu 18 za bangi, alihojiwa pamoja na watu wengine kadhaa na baadae kuachiliwa.