pmbet

Wizara ya Afya yamjibu Manara kuhusu 'Utani'

Eric Buyanza

May 16, 2024
Share :

Kupitia ukurasa wake wa Instagram leo, Haji Manara aliposti video fupi ya kipindi cha nyuma ikielezea uwepo wa homa ya Mgunda.
 

Muda mchache baadae Wizara ya Afya waliijibu post hiyo kwa maneno yafuatayo;
 

"Salamu @HajiManara. Tumeona habari hiyo ambayo inazunguka mitandaoni kuonyesha utani wa jadi wa mpira kati ya Timu za Simba na Yanga ukihusisha jina la Kocha Mgunda. Hata hivyo video hiyo uliyoiweka mtandaoni inaweza pokelewa tofauti na watu wengine na kuzua taharuki juu ya mlipuko wa ugonjwa wa Mgunda. Kutokana na ushawishi ulionao ndani ya jamii wapo watu wengine wanaweza jua kuwa ugonjwa huo umeibuka tena na sio ujumbe uliokusudia wa utani wa mpira. Ni vyema ukaelezea kuwa video hiyo ni ya muda na hakuna ugonjwa wa Mgunda nchini au kuitoa na kutumia maudhui mengine"

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet