Wizkid afuta post zote Instagram, followers wake milioni 18 hawaelewi
Eric Buyanza
April 1, 2025
Share :
Nyota wa muziki wa Nigeria, Wizkid amezua minong'ono miongoni mwa wapenzi wa muziki wake baada ya kufuta 'post' zote kwenye mtandao wake wa kijamii wa Instagram huku akiwaacha 'Followers' wake wapatao milioni 18 wakiwa hawaelewi kinachoendelea.
Kumbukumbu zinaonyesha hii sio mara ya kwanza kwa Wizkid kuchukua hatua kama hiyo kwani aliwahi kufanya hivyo Agosti 2019 na kurudia tena Julai 2022 kabla ya kutoka kwa albamu yake 'More Love, Less Ego'.