Wizkid kutumia mamilioni kusaidia watoto
Eric Buyanza
December 11, 2023
Share :
Mwanamuziki kutoka nchini Nigeria, Wizkid ameahidi kutoa misaada kwa watoto, Naira 100 milioni ambazo ni zaidi ya Tsh 316 milioni kwa ajili ya sikukuu ya Chrismass.
Wizkid ameeleza hayo kupitia Insta story yake kwa kuandika kuwa atafanya hivyo kwa ajili ya marehemu mama yake Jane Dolapo aliyefariki Agasti 18 mwaka huu jijini London Uingereza.