pmbet

Xabi Alonso mrithi wa Jurgen Klopp Liverpool

Joyce Shedrack

February 7, 2024
Share :

Klabu ya Liverpool imeanza mazungumzo na Kocha Mkuu wa Bayer Leverkusen ya nchini Ujerumani Xabi Alonso (42)  ili kurithi mikoba ya Jurgen Klopp kocha mkuu wa Liverpool aliyetangaza kuondoka klabuni hapo mwisho wa msimu huu .

 

Xabi Alonso anaonekana kuwa chaguo la kwanza la Liverpool kutokana na ubora wake aliouonyesha akiifundisha Bayer Leverkusen.

 

Bayer Leverkusen mpaka sasa ndio vinara wa Ligi kuu ya soka nchini Ujerumani (BUNDESLIGA) nyuma ya Bayern Munich huku ikiwa klabu pekee kutoka Ujerumani ambayo haijapoteza mchezo wowote katika mashindano yote timu hiyo iliyoshiriki msimu huu.

 

Alonso ambaye ni kiungo wa zamani wa Liverpool alijiunga na Bayer 04 katikati ya msimu uliopita timu hiyo ikiwa nafasi ya pili kutoka mwisho kwenye  msimamo wa Bundesliga aliisadia timu hiyo kumaliza ligi  ikiwa nafasi ya sita. 

 

Mhispania huyo aliwahi kuitumikia klabu ya Liverpool kama kiungo wa kati na kucheza michezo 210,bado anamkataba wa kuitumikia Bayer Leverkusen mpaka mwezi June mwaka 2026.

 

Makocha wengine waliopo kwenye rada za  Liverpool endapo wakikosa huduma ya Xabi Alonso ni Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Ujerumani Julian Nagelsmann, kocha mkuu wa Brighton Roberto De Zerbi na Kocha Sporting CP Ruben Amorin.

 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet