pmbet

Xabi Alonso na Fabrigas kwenye orodha ya kumrithi Guardiola.

Joyce Shedrack

February 3, 2026
Share :

Kocha wa zamani wa Real Madrid, Xabi Alonso, amejiunga na orodha ya makocha watatu wanaowindwa na Manchester City kuchukua nafasi ya Pep Guardiola.
Manchester City shortlist Xabi Alonso and two others as Pep Guardiola's  potential successor | Yardbarker

Kulingana na gazeti la Telegraph la nchini Uingereza, kuna imani inayoongezeka kwamba Guardiola ataondoka klabuni mwishoni mwa msimu huu na City tayari wameanza kuchukua hatua kwa kuchagua warithi wa nafasi hiyo.
 

Mkataba wa sasa wa Guardiola unaisha mwaka 2027, lakini Mhispania huyo anaweza kuondoka mwezi Mei.

 

Alonso yuko kwenye orodha ya makocha watatu pamoja na kocha wa zamani wa Chelsea Enzo Maresca, ambaye aliiambia Blues mara mbili kwamba alikuwa akifanya mazungumzo na City.
 

Kiungo wa zamani wa Arsenal na Kocha mkuu wa Como, Cesc Fabregas, anaaminika kuwa kwenye orodha hiyo pia. Timu yake ya Serie A iko katika nafasi ya sita na iko kwenye hatua za kufuzu kwa michuano ya Ulaya.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet