pmbet

"Xavi ameumia wachezaji wale wale Hans Flick anashinda"Laporta.

Joyce Shedrack

March 9, 2026
Share :

Mgombea urais wa Barcelona, Joan Laporta, amefunguka kuhusu kauli zilizotolewa na Xavi Hernández katika mahojiano yake na La Vanguardia akisema Xavi anaumizwa na mafanikio ya Hans Flick anayoyapata akiwa na wachezaji wale wale aliokuwa nao Xavi.

Kiungo huyo wa zamani na kocha aliushambulia vikali uongozi wa zamani, akimlaumu Laporta kwa kushindikana kurejea kwa Lionel Messi mwaka 2023, huku pia akidai kuwa mshirika wa karibu wa Laporta, Alejandro Echevarria, ndiye anayeendesha mambo ndani ya klabu.
Xavi accuses Laporta of derailing Messi return - 'Told me if Leo came back,  he would wage war on him' | Barca Universal
Laporta ameweka wazi kuwa ameumizwa na kauli za Xavi na akasisitiza kuwa uamuzi wake wa kuachana na kocha huyo wa zamani ulikuwa sahihi.

“Nilishangaa na kuumia. Ninapoona kauli hizi kutoka kwa Xavi, namfikiria Hansi Flick. Ni vigumu kuwa rais wa Barça na lazima uchukue maamuzi magumu nilifanya kile nilichopaswa kufanya,”

“Kwa Xavi, niliona kwamba tulikuwa tunaenda kupoteza, na kwa Flick ninaona kwamba tutaenda kushinda ninaelewa kwamba ameumia kwa wachezaji wale wale, Xavi alikuwa anapoteza, na Flick anashinda.”

“Haya ni maamuzi matatu magumu zaidi niliyowahi kufanya: Lionel Messi, Ronald Koeman na Xavi Hernández. Niliyafanya nikiweka maslahi ya Barça mbele. Wawili kati yao nilikuwa nao kama wachezaji, lakini haya ni maamuzi ambayo lazima yafanywe. Wote ni magwiji wa Barça".

“Barça haiwezi kuendeshwa kwa kutumia kompyuta tu; ni suala la hisia. Barça iko juu ya wachezaji na hata marais.” Amesema Laporta.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet