Xavi amvulia kofia beki kitasa aliyemzuia Mbappe
Sisti Herman
April 11, 2024
Share :
Mara baada ya kushinda mchezo wa robo fainali ya kwanza ya ligi ya mabingwa Ulaya dhidi ya PSG kwa 3-2, kocha wa Barcelona Xavi Hernandez amemwagia maua mengi sana beki wake wa kati Kinda Pau Cubarsí kwa kumzuia mshambuliaji bora zaidi kwasasa duniani Kylian Mbappe kwa kiwango kikubwa.
"Cubarsí ni mchezaji wa ajabu. Amekuwa wa kiwango cha dunia, sio kawaida katika miaka 17 kufanya hivyo!", Xavi anasema.
“Niliishiwa na maneno ya kumsifu. Yuko katika kiwango cha kipekee, anashindana kama mchezaji mzee. Ni ajabu aisee.
Alimaliza hivyo kumsifia beki huyo mwenye umri wa miaka 17 ambaye ameweka rekodi ya beki wa kati kinda zaidi kucheza UEFA.
Kwenye mchezo huo uliomalizika kwa Barca kushinda 3-2 ugenini magoli yalikungwa na Raphinha aliyefunga mawili na Christensen kwa upande wa Barca, huku kwa upande wa wenyeji PSG yakifungwa na Vitinha na Osmane Dembele.