pmbet

Yacouba kurejea tena Bongo

Eric Buyanza

December 8, 2023
Share :

Nyota wa zamani wa Yanga na Ihefu, Yacouba Songne yupo mbioni kurejea nchini ambapo ukurasa huu umethibitisha kuwa yupo kwenye mawasiliano ya karibu kumalizana na klabu ya Geita Gold ambao wamejiongeza kwa kumuita mezani mshambuliaji huyo anayecheza soka la kulipwa Djibouti ili kumsajili kupitia dirisha dogo la usajili litakalofunguliwa wiki ijayo.
 

Taarifa zilizothibitishwa na pande zote mbili zinasema, Geita inayosaka washambuliaji wawili wa kukiongezea nguvu kikosi hicho kinachoshiriki Ligi Kuu wameshaanza mazungumzo hayo na nyota huyo wa zamani wa Asante Kotoko ya Ghana.
 

Yacouba anayeitumikia Arta Solar7 ya Djibouti anataka kuondoka nchini humo baada ya kuona soka la nchi hiyo ni laini likikosa ushindani mkubwa kama ambavyo alitegemea huku akiwa kwenye kiwango kizuri tu tangu atue nchini humo ameshafunga mabao manane.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet