pmbet

Yajue magari 6 yaliyotumiwa na Mwalimu Nyerere

Eric Buyanza

February 5, 2024
Share :

Makumbusho ya Dar es Salaam, imehifadhi magari sita yaliyotumiwa na Mwalimu  Julius Nyerere, wakati wa uhai wake, likiwemo gari ambalo lilitumika katika awamu tatu za uongozi. Kwa mujinu wa mhifadhi wa makumbusho, Pius Gondeka amesema magari yote kila moja lina historia yake.

ROLLS ROYCE
Ilitengenezwa Uingereza mwaka 1938 na lilifika Tanganyika mwaka 1962, lilitumiwa na viongozi mbalimbali ktk shughuli za kiserikali, kupokea wageni mashuhuri waliokuja kutembelea Tanganyika. Baadhi ya viongozi waliofika na kulitumia gari hilo ni pamoja na Mfalme wa Ethiopia, hayati  Haille Selasie, Rais wa Liberia, William Tubman,  Gavana wa mwisho Sir Richard Turnbull.

ROLLS ROYCE (PHANTOM V)
Ilitumiwa na Mwalimu Nyerere mwaka 1970 kuwapokea viongozi wa nchi mbalimbali walioitembelea Tanzania. Gari hilo limetumiwa pia na Rais wa Awamu ya Pili, Mzee Ali Hassan Mwinyi na Rais wa Awamu ya Tatu, hayati Benjamin Mkapa. Gari hilo lina sehemu mbili za kuweka bendera mbele, ambapo upande wa kulia anakaa Rais mgeni aliyewasili na kuwekwa bandera ya nchi yake na kwa upande wa kushoto anakaa Rais mwenyeji na bendera ya Tanzania. Anasema sehemu ya juu ya gari inaweza kufunguliwa na kuwa wazi, endapo viongozi watasimama kusalimia ama kupunga mikono kwa wananchi. “Gari hiyo ilipendwa sana kwa wakati ule, ndio gari ilionekana ina nguvu zaidi, gari ya hadhi, heshima na kuonesha kujali wageni,” amesema.

MERCEDES BENZ E 300
Gari hilo limetengenezwa Ujerumani na kununuliwa Desemba 17, 1996 na lilitumiwa na Mwalimu ktk shughuli mbalimbali, hususani baada ya  kustaafu. Gari hii  ni ya mwisho kutumiwa na Mwalimu kipindi cha uhai wake. Septemba 24, 2004 mjane wa Baba wa Taifa, Mama Maria Nyerere aliitoa gari hiyo kwa Makumbusho ya Taifa.

MERCEDES-BENZ  230.6
litumika katika shughuli za serikali, wakati wa  Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), ilipoanza mwaka  1967 na kuvunjika mwaka 1977 kwa sababu mbalimbali.

AUSTIN MORRIS (A40 VAN GUARDS) 
Hii ilitengenezwa Uingereza kati ya mwaka 1945 -1950, ambayo aliitumia katika shughuli za chama cha TANU na harakati za kudai Uhuru.

AUSTIN MORRIS (MINOR)
Hili lilitumika wakati wa harakati za kupigania uhuru na ilitengenezwa  Uingereza kati ya mwaka 1940-1950

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet