pmbet

Yamal agomea ndege ya Barcelona, akodisha ya binafsi kwenda London

Eric Buyanza

October 23, 2026
Share :

Klabu ya Simba imetozwa faini ya Tsh milioni kumi kwa kosa la mashabiki wake kurusha chupa uwanjani tukio ambalo walifanya zaidi ya mara moja kwenye mchezo wa dabi ya Kariakoo uliopigwa mnamo Oktoba 10, 2026 katika uwanja wa Uhuru Dar es Salaam na kumalizika kwa Simba SC kuibuka na ushindi wa 2-1.

 

Adhabu hiyo imetolewa na Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) kupitia taarifa yake ya Oktoba 21, 2026 ambayo imeeleza kuwa kosa hilo limekuwa la kujirudia kwa Mashabiki wa Simba ndani ya msimu wa 2026/2027 kwani mashabiki hao pia walifanya kosa mfanano na hilo kwenye mchezo dhidi ya Pamba Jiji.
 

Aidha Simba SC imetozwa faini ya Tsh milioni tano kwa kosa la mashabiki wake kuvamia eneo la kuchezea wakati mchezo unaendelea na mmoja kati yao alimfuata kijana mwokota mpira (Ball kids) na kumfanyia fujo tukio ambalo lilidhibitiwa na walinzi wa uwanja.
 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet