pmbet

Yamal amepiga hatua kuliko Messi na Ronaldo wakiwa na miaka 19 - Gerald

Eric Buyanza

November 10, 2026
Share :

Kiungo wa zamani na nahodha wa kihistoria wa Liverpool, Steven Gerrard, ametoa kauli iliyotikisa ulimwengu wa soka kwa kudai kuwa chipukizi wa FC Barcelona, Lamine Yamal, amepiga hatua kubwa kisoka (more advanced) kuliko walivyokuwa Lionel Messi na Cristiano Ronaldo wakiwa na umri wa miaka 19.

 

Kauli hiyo ya Gerrard inakuja huku Yamal akiendelea kuonyesha kiwango cha hali ya juu kilichomfanya kuwa mmoja wa mastaa wakubwa duniani kwa sasa.

Gerrard, ambaye alicheza dhidi ya Messi na Ronaldo walipokuwa vijana, alitoa maoni hayo kwenye kipindi cha podikasti ya The Overlap.

 

Gerrard ameeleza kuwa vitu anavyovifanya Yamal uwanjani akiwa na umri huo wa ujana ni vya kutisha na hajawahi kuviona kwa mchezaji mwingine yeyote wa umri wake.

 

"Katika masuala ya kipaji na uwezo, anafanya vitu uwanjani ambavyo sijawahi kuona kijana wa miaka 19 akivifanya. Nadhani amepiga hatua zaidi kuliko alivyokuwa Ronaldo akiwa na miaka 19. Na pia yuko mbele kuliko Messi alivyokuwa katika umri huo," alisema Gerrard.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet