pmbet

Yamal na Mbappé ndio warithi wa Messi na Ronaldo - Guardiola

Eric Buyanza

November 27, 2026
Share :

Kocha wa zamani wa Manchester City na FC Barcelona, Pep Guardiola, amewataja nyota wa Barcelona, Lamine Yamal, na mshambuliaji wa Real Madrid, Kylian Mbappé, kuwa ndio wachezaji wawili wenye uwezo wa kuchukua nafasi ya ufalme wa soka duniani kutoka kwa wakongwe Lionel Messi na Cristiano Ronaldo.

 

Akizungumza katika mahojiano maalum na mshambuliaji wa zamani wa timu ya taifa ya Brazil, Romário, kupitia chaneli yake ya YouTube ya RomarioTV, Guardiola alisema kuwa wakati Messi na Ronaldo wakielekea ukingoni mwa maisha yao ya soka baada ya wote wawili kustaafu kucheza timu zao za taifa kizazi kipya kinaanza kuchukua hatamu.

 

"Nadhani Lamine ana kitu cha tofauti. Ndiyo, huyu kijana ni wa kipekee. Na ana ile shauku ya kutaka kuwa bora zaidi, jambo ambalo ni muhimu sana," alisema Guardiola.

 

Mbali na Yamal, kocha huyo raia wa Hispania alimtaja Kylian Mbappé (27) kama mrithi mwingine wa uhakika kutokana na uwezo wake wa kudumu katika kiwango cha juu kwa miaka mingi sasa.

 

"Ni vigumu, lakini nadhani Lamine ni mmoja wao... na bila shaka, Mbappé, ambaye tayari amekuwa katika kiwango hicho cha juu kwa miaka mingi sasa," aliongeza Guardiola.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet