Yanga dimba leo ASFC, Hauising watashikilia bomba?
Joyce Shedrack
January 30, 2024
Share :
Bingwa mtetezi wa kombe la shirikisho la Azam Sport Federation Cup (ASFC) Yanga Sports Club leo anaanza safari ya kulitetea taji hilo ambalo lipo mikononi mwao kwa misimu miwili mfululizo .
Klabu ya Yanga itashuka dimbani majira ya saa moja usiku kucheza na Hausung fc ambao ni mabingwa wa Mkoa wa Njombe ndani ya uwanja wa Azam Complex Chamazi, katika mchezo wa hatua ya 32 bora ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC)
Baada ya mashabiki wa Yanga kukaa muda mrefu bila kuiona timu yao ikicheza tangu ilipotolewa kwenye Kombe la Mapinduzi, Januari 7, leo itarejea uwanjani huku ikiwakosa nyota wake 7 ambao ni Dickson Job,Bakari Mwamnyeto,Ibrahim Bacca,Kennedy Musonda,Mudathiri Yahya,Djigui Diarra na Stephan Aziz Ki.
Kocha mkuu wa Hausung amesema Shangwe Michael alisema wanaiheshimu Yanga na watacheza kwa tahadhari kubwa na wamewafanyia kazi mastaa wote wa Yanga haswa Pacome ambaye wanajua staili yake ya uchezaji.
“Tutacheza kwa kuwaheshimu na lengo ni kushinda kwani hatua hii ni ya mtoano usiposhinda unatolewa,” amesema kocha Shangwe.