pmbet

Yanga kuanzia hatua ya awali, Simba kuanzia raundi ya pili CAF

Sisti Herman

July 11, 2024
Share :

Droo ya michuano ya klabu ya Shirikisho la soka barani Afrika (CAF) itachezeshwa rasmi leo mchana huku Tanzania ikiwakilishwa na timu nne (4), Yanga na Azam kwenye ligi ya Mabingwa Afrika na Simba na Coastal Union kwenye kombe la shirikisho Afrika.

Klabu za Yanga, Azam na Coastal Union zitaanzia hatua ya awali ya mchujo kufuzu hatua ya makundi ya michuano ya CAF huku klabu ya Simba ikianzia raundi ya pili kuwania kufuzu hatua ya makundi ya kombe la shirikisho Afrika.

Katika droo hiyo wawakilishi wa Tanzania kwenye ligi ya Mabingwa Afrka, Azam na Yanga wanaweza kukutana wao kwa wao au moja kati ya timu hizi;

- Gor Mahia (Kenya)
- APR (Rwanda)
- Vital O (Burundi)
- El Merriekh (Sudan)
- SC Villa (Uganda)
- CBD (Ethiopia)
- Dekadaha (Somalia)
- Arta Solar ( Djibouti)

Wawakilishi wa Tanzania kwenye kombe la shirikisho Coastal Union watakutana na moja kati ya hizi timu;

- Bravo (Angola)
- Orapa United (Botswana)
- CD Luanda (Angola)
- Black Bulls (Msumbiji)
- Dynamos (Zimbwabwe)
- Stellenboch (Afrka kusini)
- De Augusto (Gueine ya Ikweta)
- Alice Port (Comorro)
- Hotspurs (Eswatini)
- Elgeco/Forester (Shelisheli)

Kila la kheri kwa timu za Tanzania.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet