Yanga kucheza na Red Arrows siku ya Wananchi
Sisti Herman
July 29, 2024
Share :
Klabu ya Yanga imetangaza rasmi kucheza na Mabingwa wa Darport Kagame Cup 2024 klabu ya Red Arrows ya Zambia kwenye kilele cha siku ya wananchi kwenye dimba la Benjamin Mkapa siku ya tarehe 4 Agosti.
Hayo yamesemwa na Haji Manara kwenye mkutano na waandishi wa habari ulioitishwa na idara ya Habari na Mawasiliano ya klabu hiyo Makao makuu ya klabu hiyo mtaa wa twiga na Jangwani, Kariakoo Dar es salaam.