pmbet

Yanga kuipeleka Dodoma Zanzibar

Sisti Herman

June 15, 2025
Share :

 

Mechi ya Ligi Kuu kati ya wenyeji Yanga dhidi ya Dodoma Jiji iliyopangwa Juni 22 huenda ikachezwa kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar endapo mambo yataenda kama yalivyopangwa awali.

Hatua ya mechi hiyo kupelekwa Zanzibar inaelezwa ni kutokana na Uwanja wa KMC Complex ambao inautumia Yanga kwa mechi za nyumbani kutumiwa na watani zao Simba watakaoikaribisha Kagera Sugar tarehe husika.

Taarifa kutoka Bodi ya Ligi Kuu (TPLB), zimenidokeza mechi hiyo iko mbioni kupelekwa Zanzibar ikiwa ni siku tatu kabla ya kikosi hicho kurejea Dar es Salaam kucheza na Simba Juni 25 katika pambano la Dabi ya Kariakoo.

Mechi dhidi ya Dodoma Jiji ilikuwa ya mwisho kwa Yanga msimu huu kwenye ligi, lakini sasa ni ya pili kutoka mwisho baada ya kutangazwa Dabi ya Kariakoo itachezwa Juni 15 kutoka Juni 15 iliyotangazwa, Ingawa Simba Bado Hawajathibitisha Kushiriki Mechi Hiyo.

Taarifa zinaeleza Yanga ilipanga kucheza na Dodoma Jiji Juni 22 Zanzibar ikiwa ni sehemu ya kuweka kambi pia hadi Juni 28 itakapocheza fainali ya Kombe la Shirikisho (FA) dhidi ya Singida Black Stars.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet