Yanga kutema Ma ‘Pro’ wanne, hawa watajwa
Eric Buyanza
December 11, 2023
Share :
Klabu ya Yanga inasemekana inategemea kuachana na wachezaji wa kimataifa wanne walioshindwa kutoa ushindani mkubwa kwenye kikosi cha timu hiyo na kushindwa kupata nafasi ya kucheza.
Kwenye orodha ya wachezaji iliyofika kwenye dawati letu la habari wanatajwa mastaa wanne ambao ni Gift Fred raia wa Uganda, Hafiz Konikoni raia wa Ghana, Mahlatse Makudubela raia wa Afika kusini na Jesus Moloko raia wa Congo DR.
Yanga pia inahusishwa na mastaa tofauti kwenye soko la usajili kama mshambuliaji wa Asec Mimosa Sankara Karamoko, mshambuliaji wa Douala Dynamos Lionel Ateba na wengine wengi.