Yanga kuumana na Kaizer Chiefs kuania Toyota Cup leo
Sisti Herman
July 28, 2024
Share :
Klabu ya Yanga leo saa 10 jioni itashuka dimbani dhidi ya klabu ya Kaizer Chiefs kwenye dimba la Toyota jijini Johannesburg nchini Afrika kusini kuwania kombe la Toyota Cup wakiendelea maandalizi ya msimu mpya nchini humo. Yanga watavaana na Chiefs kuwania taji hilo baada ya kukosa taji la Mpumalanga Cup ambalo limetwaliwa na TX Galaxy baada ya kuwafunga Augsburg ya Ujerumani juzi.
Mechi hiyo itawakutanisha kocha wa sasa wa Yanga Miguel Gamondi na mtangulizi wake Nasredinne Nabi.