Yanga kuungana na Azam fainali Babati
Sisti Herman
May 19, 2024
Share :
Baada ya jana klabu ya Azam kutangulia kwenye fainali ya michuano ya kombe la shirikisho nchini (CRDB Federation Cup) kwa kuwachapa Coastal Union 3-0 kwenye nusu fainali ya kwanza jijini Mwanza, leo klabu ya Yanga itashuka kwenye dimba la Sheikh Amri Abeid jijini Arusha kucheza mchezo wa nusu fainali ya pili dhidi ya klabu ya Ihefu.
Mshindi wa mchezo wa leo ataungana na Azam kucheza fainali ya michuano hiyo ambayo itachezwa kwenye dimba la Tanzanite Kwaraa mjini Babati, Manyara.