"Yanga lipeni deni ili msajili" - FIFA
Sisti Herman
June 19, 2024
Share :
Dirisha la usajili msimu wa 2024/2025 kwa Klabu za Ligi Kuu ya NBC (NBCPL), NBC Championship (NBCCL), First League (FL) na Ligi Kuu ya Wanawake (TWL) limefunguliwa Juni 15, 2024.
Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) pamoja na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF) imezifungia klabu zifuatazo kusajili mpaka zitakapowalipa wachezaji wanaozidai;
1. Young Africans
2. Singida Fountain Gate FC
3. Tabora United FC
4. Biashara United FC
5. FGA Talents FC
Klabu ambayo itawalipa wahusika, itaondolewa mara moja adhabu ya kufungiwa kusajili.
Hadi leo asubuhi kupitia mumo wa FIFA (FIFA legal portal) hakuna taarifa ya klabu yoyote kati ya hizo iliyowalipa wahusika.