pmbet

"Yanga mshukuruni Mo Dewji, mlilala usingizi wa Pono" - Ahmed Ally

Sisti Herman

February 26, 2024
Share :

Hizi ni nukuu za Meneja wa idara ya habari wa klabu ya Simba Ahmed Ally kwenye mkutano wana wanahabari kwaajili ya kuzindua wiki ya hamasa kwaajili ya mchezo wa raundi ya mwisho ya hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa Afrika dhidi ya Jwaneng' Galaxy utakaochezwa uwanja wa Benjamin Mkapa siku wikiendi ijayo.

 

“Kufuzu kwa Yanga SC katika hatua ya robo fainali wa kushukuriwa ni Rais wa heshima wa Simba ni Mohammed Dewji na wa pili ni Simba SC. Wakati Mo anakuja kuwekeza Simba alisema vision yake ni kushinda ubingwa wa Afrika na baada ya hapo tukaanza mchakato wa kutawala soka la Afrika.Wakati Mohammed Dewji anatengeneza dira ya kutawala soka la Afrika vilabu vingine vilikuwa vimelala usingizi wa pono, vilikuwa haviwazi kushindana Afrika na kusumbua"

"Baada ya miaka mitano ndio na wengine wameamka na wenyewe kutaka kuanza kufanya vizuri. Kama Simba SC na Mohammed Dewji tungeendelea kulala basi hadi sasa hakuna klabu yoyote Tanzania ingekuwa na hasira, malengo ya kufanya vizuri kwenye michuano ya Afrika ndio maana nasema robo fainali yao ya kwanza wa kushukuriwa ni Mohammed Dewji ndio aliwaamsha watu kutoka kwenye usingizi. Huu ndio ukweli ambao utadumu milele.”- Ahmed Ally.

 

Fuatilia mkutano huu live kupitia PMTV Youtube

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet