Yanga na Azam kukutana Babati
Sisti Herman
April 17, 2024
Share :
Droo ya robo fainali ya kombe la shirikisho la TFF linalodhaminiwa na benki ua CRDB (CRDB FC) imechezeshwa leo ambapo kati ya wababe nane waliotinga hatua hiyo kila timu imeshajua itakutana na ipi.
Kwenye droo hiyo iliyochezeshwa na magwiji wa zamani wa soka la Tanzania Said Maulid (SMG) na George Lucas (Gaza) ikisimamiwa na Meneja wa mashindano wa TFF Baraka Kizuguto;
- Azam FC vs Namungo FC
- Yanga SC vs Tabora United
- Coastal Union vs Geita Gold
- Ihefu SC vs Mashujaa
Baada ya droo hiyo washindi wa mechi hizi watakutana nusu fainali ambayo itakuwa;
- Azam/Namungo vs Ihefu/Mahujaa
- Yanga/Tabora vs Coastal/Geita
Baada ya droo hiyo maoni ya wadau wengi wametabiri kuwa timu za Azam na Yanga zitakutana fainali itakaypochezwa uwanja wa Tanzanite Kwaraa Babati, Manyara.
Pia droo hiyo imeshuhudiwa na wawakilishi wa timu hizo.