pmbet

Yanga na JKT yaahirishwa kisa uwanja kujaa maji

Sisti Herman

April 23, 2024
Share :

Mchezo wa ligi kuu Tanzania bara kati ya JKT Tanzania dhidi ya Yanga SC uliopangwa kuchezwa leo kwenye uwanja wa Meja Jenerali Isamuyo umeahirishwa kuchezwa baada ya kamisaa wa mchezo kujiridhisha uwanja hauna sifa za kutumika baada ya kujaa maji kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar Es Salaam.

“Baada ya kujiridhisha uwanja bado umejaa maji na hivyo kutokana na kanuni mchezo hauwezi kuchezwa , kwa hiyo taarifa rasmi itatoka ni lini mchezo huu utachezwa baada ya sasa tunaenda kukukutana na kujadiliana kwa undani nini tufanye" amesema Kamisaa wa mchezo wa JKT dhidi ya Yanga, Kamwanga Tambwe.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet