Yanga na Kagoma mambo fresh
Sisti Herman
May 5, 2024
Share :
Klabu ya Yanga inatajwa kuwa kwenye hatua za mwisho kumaliza usajili wa aliyekuwa kiungo wa Geita Gold na Singida FGFC Yussuph Kagoma ambaye hajaichezea timu yake kwa karibu miezi mitatu sasa.
Kagoma ambaye inasemekana alisaliwa na mkataba wa msimu mmoja mbele atajiunga Yanga kama Yanga watalipa kiasi cha fedha kinachoweza kuvunja mkataba wake Singida.