Yanga na Simba kupigwa Aprili 20
Sisti Herman
April 7, 2024
Share :
Bodi ya ligi kuu Tanzania bara (TPLB) imeupangia tarehe rasmi mchezo namba 180 wa ligi hiyo kati ya Yanga na Simba ambao utachezwa siku ya tarehe 20 mwezi huu wa nne saa 11 kamili jioni kwenye dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.
Mchezo huo unaotajwa kama wa maamuzi kwenye mbio za ubingwa wa ligi hiyo unaenda kuchezwa huku timu hizo za kariakoo zikiwa zimetoka kuondolewa kwa pamoja kwenye michuano ya ligi ya mabingwa Afrika kwenye hatua ya robo fainali.
Yanga wanaongoza ligi hiyo wakiwa na alama 52 baada ya kucheza michezo 20 huku Simba wakiwa nafasi ya tatu wakiwa na alama 45 baada ya kucheza michezo 19.
Je nani ataibuka mshindi?