Yanga ni mwendo wa 5G tu, watambulisha mashine ya mabao Chamazi
Sisti Herman
January 30, 2024
Share :
Klabu ya Yanga imeanza ilipoishia kwenye michuano ya ASFC baada ya kuwabamiza 5-1 Hausing Fc kutokea mkoani Njombe nakuanza vyema kampeni ya kutetea taji hilo kwa msimu wa tatu mfululizo.
Magoli ya Yanga kwenye mchezo huo yamefungwa na mshambuliaji wao kinda Clement Mzize alitupia matatu kwenye nyavu huku Makhlase Makudubela “Skudu” na Jonas Mkude wakitupia mojamoja nyavuni.
Klabu hiyo pia imetumia mchezo huo kumtambulisha mshambuliaji wao mpya Joseph Guede waliyemsajili dirisha dogo lililotamatika Januari 15.