Yanga njia nyeupe CAF, wapinzani wao wajileta Chamazi
Sisti Herman
July 25, 2024
Share :
Klabu ya Vital’O ya Burundi imeuidhinisha uwanja wa Azam Compelx kuwa uwanja wao wa nyumbani kwenye mechi za hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Yanga baada Burundi kukosa uwanja ulioidhinishwa kwa ajili ya mechi za CAF.
Yanga wamepangwa kuvaana na Vital’O FC ya Burundi kwenye mchezo wa hatua ya awali Ligi ya Mabingwa Afrika, ambapo Yanga itaanzia ugenini lakini itacheza mechi zote mbili ndani ya ardhi ya Tanzania.
Mchezo wa mkondo wa kwanza unatarajiwa kupigwa Agosti 16-18 katika dimba la Benjamin Mkapa huku mkondo wa pili ukipigwa Agosti 23-25 mwaka huu katika dimba la Azam Complex, Chamazi.